IQNA – Rais wa Marekani, Donald Trump, ameonyesha hasira dhidi ya kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani kufuatia ukosoaji wake kuhusu vita vinavyoendeshwa na Marekani.
Habari ID: 3482139 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/13
IQNA-Rais Donald Trump wa Marekani amesema Wawakilishi wanawake katika bunge la nchi hiyo, ambao ni Waislamu, Ilhan Omar na Rashida Tlaib wanapaswa kurudishwa "walikotoka" baada ya wabunge hao wawili wa chama cha upinzani cha Democratic kupiga kelele na kulalamika wakati wa hotuba ya karibuni ya Trump katika Kongresi.
Habari ID: 3482004 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/27
IQNA-Ilhan Omar mwakilishi Mwislamu wa Bunge la Marekani, akijibu tuhuma za Donald Trump dhidi yake, alimtaja Trump kama mnyanyasaji kingono wa watoto, akisema kuwa tuhuma anazotoa mtawala huo wa Marekani dhidi yake ni jaribio la kugeuza mawazo ya umma kutoka kwenye kashfa ya Jeffrey Epstein.
Habari ID: 3481928 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/13
IQNA – Meya wa Jiji la New York, Zahran Mamdani, ametetea agizo lake linaloweka mipaka kwa ukamataji unaofanywa na maafisa wa Idara ya Uhamiaji na Forodha ya Marekani (ICE), akieleza kuwa ulinzi wa wahamiaji si suala la kisera pekee, bali ni wajibu wa kimaadili unaochochewa na mafundisho ya Qur’ani Tukufu na Hijra ya Mtume Muhammad (rehema na amani ziwe juu yake) kwenda Madina.
Habari ID: 3481900 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/08
IQNA – Mjumbe wa Baraza la Kisiasa la harakati ya Nujaba ya Iraq amesema kuwa tishio lolote dhidi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, linachukuliwa kuwa ni tangazo la vita.
Habari ID: 3481828 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/21
IQNA-Wanazuoni na wasomi wa Ulimwengu wa Kiislamu, katika taarifa yao, wameonyesha kuunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khamenei, kufuatia machafuko ya hivi karibuni nchini, huku wakitoa tamko linalomtaja rais Trump wa Marekani kama mtu “muhrib”
Habari ID: 3481811 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/17
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kundi la watu waharibifu Alhamisi usiku mjini Tehran waliharibu mali za umma na za wananchi kwa ajili ya kumfurahisha rais wa Marekani huku akisisitiza kuwa Iran haitalegeza msimamo katika kukabiliana na magenge ya wahalifu.
Habari ID: 3481785 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/10
IQNA- Meya wa jiji la London, Sadiq Khan, amemjibu kwa ukali Rais wa Marekani Donald Trump, akimtuhumu kuwa “mbaguzi wa rangi, jinsia, wanawake na mwenye chuki dhidi Uislamu” baada ya Trump kutumia hotuba yake katika Umoja wa Mataifa kumuita Khan “meya mbaya” na kudai kuwa jiji la London linaelekezwa kwenye “sheria ya Kiislamu (sharia)”.
Habari ID: 3481286 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/26
IQNA – Mjumbe wa chama cha Democratic katika Bunge la Marekani, Bi Ilhan Omar, amesisitiza utambulisho wake wa Kiislamu, akisema anajivunia kuwa Mwislamu.
Habari ID: 3481264 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/21
IQNA – Shirika moja la utetezi wa haki limeshutumu agizo jipya kutoka kwa serikali ya Trump linalozuia utoaji wa misaada ya majanga kwa majimbo na miji ya Marekani inayopinga bidhaa na makampuni ya Israel yanayoshiriki katika uhalifu wa kivita, likilitaja kuwa si la kizalendo, linakiuka katiba, na ni shambulio dhidi ya haki za binadamu na uhuru wa kujieleza.
Habari ID: 3481048 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/07
IQNA-Harakati ya Mpambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imekariri upinzani wake dhidi ya matamshi yaliyotolewa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu suala la kuwahamusha makazi Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza kwa kisingizio cha kulijenga upya eneo hilo.
Habari ID: 3480213 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/13
Kadhia ya Palestina
Trump kupoteza dau lake kuhusu Gaza, asema mchambuzi
IQNA – Mchambuzi kutoka Tunisia anasema kwamba Rais wa Marekani Donald Trump atashindwa katika dau lake kuhusu Gaza kwani mpango wake wa kuwafurusha Wapalestina kutoka eneo lililozungukwa umepokelewa kwa upinzani mkubwa.
Habari ID: 3480202 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/12
Waislamu
IQNA - Akizungumza siku moja kabla ya uchaguzi wa rais wa Marekani unaofanyika leo, rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alidai Waislamu wanajua urais wa Kamala Harris utakuwa hatari kwao.
Habari ID: 3479705 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/05
Muungano wa makundi ya Waislamu wa Marekani ulisisitiza kuwa Joe Biden na Donald Trump ni "wagombea walio na dosari mbaya," wakibainisha kwamba utawala ujao unapaswa kuweka "utakaso wa kikabila wa Wapalestina" kama mstari wake mwekundu.
Habari ID: 3479047 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/07/01
Ubaguzi wa Rangi’
Maoni ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kuhusu Wapalestina yamepingwa na majina ya kutetea haki za binadamu kuwa ya "kibaguzi.
Habari ID: 3479037 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/06/30
WASHINGTON, DC (IQNA) - Donald Trump aliuambia mkutano wa wafadhili wa Kiyahudi wa Republican siku ya Jumamosi kwamba atarejesha marufuku yake ya wasafiri kutoka nchi nyingi za Waislamu ikiwa atashinda tena urais mnamo 2024.
Habari ID: 3477806 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/29
TEHRAN (IQNA) - Mshauri wa sera za kigeni wa Spika wa Bunge la Iran ameashiria mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ambaye aliuawa kigaidi kufuatia amri ya rais Donald Trump wa Marekani na kusema, Trump ni gaidi nambari moja duniani.
Habari ID: 3473315 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/31
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haiimaini Marekani hata kidogo na uzoefu mchungu wa mazungumzo yaliyotangulia na Marekani katika fremu ya JCPOA kamwe hautarudiwa tena kwani hakuna taifa lolote huru na lenye akili litakubali kufanya mazungumzo chini ya mashinikizo."
Habari ID: 3472000 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/13
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria baadhi ya matamshi kuhusu Iran kuendelea kuwepo katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na nchi tatu za Ulaya na kusisitiza kuwa: "Kuhusu kufanya mazungumzo na nchi tatu za Ulaya, haipaswi kuziamiani na katika kila mapatano lazima kuwepo dhamana ya kweli na ya kivitendo la sivyo haiwezekani kuendelea kwa hali iliyopo."
Habari ID: 3471502 Tarehe ya kuchapishwa : 2018/05/09
TEHRAN (IQNA)-Mahujaji kutoka Marekani, Uingereza na Canada walioshiriki katika Ibada ya Hija wamebainisha wasiwasi wao kuhusu sera za chuki dhidi ya Waislamu za Rais Donald Trump wa Marekani.
Habari ID: 3471154 Tarehe ya kuchapishwa : 2017/09/03